By TCD Digital reporter.
Gavana wa kaunti ya Kitui Julius Malombe amemtaka Spika wa Bunge la Kaunti Kevin Kinengo na kundi la wawakilishi wadi wanaomuunga mkono kuacha udanganyifu wa kisiasa na kuomba msamaha hadharani kwa kumdharau na kumvunjia heshima yeye pamoja na baraza lake la mawaziri
Bila kutaja majina, Dkt. Malombe amesema ni jambo lisilokubalika kwa viongozi kusimama kwenye majukwaa ya umma, kumzungumzia vibaya na kusababisha migawanyiko katika kaunti, kisha kwa siri kuhudhuria mikutano yake wakijifanya kuomba uvumilivu na msamaha.
Gavana huyo, ambaye hakuficha hisia zake, alicheka juhudi za mwakilishi wa wadi ya Nzambani, Kitui Mashariki Joseph Mbite, za kuomba msamaha kwa niaba yake na bunge kwa kuanzisha vita dhidi ya Malombe na serikali yake hapo awali.
“Huwezi kusimama mbele yangu hapa na kudhani unajutia na kuonyesha huruma na ustaarabu. Nenda uwaambie wale unaowawakilisha kufanya jambo la heshima kwa kuomba msamaha wa kweli hadharani kwa kiwango sawa walichonitusi,” Malombe alimwambia Mbite waziwazi kwenye mazishi katika kijiji cha Kiluilu, wadi yake.
Discover more from The County diary
Subscribe to get the latest posts sent to your email.