MISS FRIDAH MAKASI ATANGAZA KUWANIA KITI CHA WOMEN REP KITUI 2027

A80096e7 1128 488a 8dd1 Dd27a2b76604

Mwanasiasa chipukizi Miss Fridah Makasi ametangaza rasmi azma yake ya kuwania kiti cha Mwakilishi wa Wanawake (Women Representative) katika Kaunti ya Kitui katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Hatua hiyo inajiri wakati kiti hicho kinashikiliwa na Irene Kasalu, ambaye tayari ameweka wazi nia yake ya kuwania kiti cha Ugavana wa Kitui mwaka huo ujao wa 2027.

Akizungumza na wafuasi wake, Miss Fridah alisema kuwa ameamua kujitosa katika kinyang’anyiro hicho ili kuwatetea wanawake, vijana na makundi maalum katika kaunti ya Kitui. Alisisitiza kuwa ana maono mapya ya maendeleo, hasa katika sekta ya uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, elimu kwa wasichana na uboreshaji wa huduma za kijamii.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa siasa za eneo hilo, kinyang’anyiro cha Women Rep Kitui kinatarajiwa kuwa na ushindani mkali, huku baadhi ya viongozi waliotajwa kuwa wagombea wakionekana kusuasua katika maandalizi yao ya awali.

Miss Fridah ameanza mikutano ya mashauriano katika maeneo mbalimbali ya kaunti akiahidi kuendesha siasa safi na shindani. Alitoa wito kwa vijana na wanawake kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia.

Wachunguzi wa masuala ya siasa za Kitui wanaona kuwa mabadiliko ya uongozi katika nafasi ya Women Rep yanaweza kuleta sura mpya katika siasa za kaunti hiyo kuelekea 2027.

Je, Miss Fridah ataweza kujizolea uungwaji mkono wa kutosha? Muda ndio utakaotoa majibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Verified by MonsterInsights